Katika mkutano mkuu wa wadau wa Parachichi wenye kaulimbiu ‘Parachichi Bora, Masoko Imara kwa Uchumi Endelevu!’, Mkurugenzi Mkuu wa Mazaohub Bwana Geophrey Tenganamba aliweza kushiriki kama mchangiaji pekee wa mada kutoka sekta binafsi kuwakilisha #MazaoHub Sisi #MazaoHub tukiwa kama mdau muhimu anayewezesha sekta ya kilimo kupitia huduma za ugani kwa njia ya kidijitali, Mkurugenzi alieleza jinsi mfumo jumuishi wa MazaoHub unavyoboresha uzalishaji na ubora wa zao la parachichi, sambamba na kusaidia wakulima kufikia masoko ya ndani na nje ya nchi kwa viwango vinavyohitajika. Cc;MazaoHub ,Hussein Bashe ,Cereals and Other Produce Regulatory Authority ,@Tanzania horticultural association (TAHA), Geophrey Tenganamba , Ministry of Agriculture